• HABARI MPYA

  Tuesday, February 15, 2022

  SERIKALI YAAGIZA TFF IWAKUTANISHE MAREFA NA TAKUKURU

  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa jana ametoa maelekezo mazito kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yanayolenga kuboresha mchezo wa mpira wa miguu nchini.
  Maelekezo hayo ameyatoa katika mkutano wa Waandishi wa Habari aliofanya katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao na Viongozi wa TFF, BMT na watendaji wa Wizara.
  Amefafanua kuwa Serikali ipo katika mikakati kabambe ya kuboresha miundombinu ya michezo katika shule 56 nchini ikiwa ni pamoja na kufunga mashine za kisasa za kufuatilia michezo (VAR) kwenye viwanja vitano kwa kuanzia pamoja na kujenga vituo vikubwa vya michezo.


  Akitoa maelekezo ya Serikali, Mhe. Mchengerwa amesema BMT ikutane na TFF mara moja kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria na taratibu za mchezo huo pendwa nchini ambapo pia amesisitiza kuwa Kamati inayohusika na Waamuzi ijitafakari kwa kuwa hadi sasa kwenye msimu huu wa ligi tayari imeshawaondoa waamuzi 13 kwa makosa ya upendeleo na rushwa.
  Mhe.Mchengerwa amesema, TFF ikutane na waamuzi wote ili kupata uvumbuzi wa changamoto na sintofahamu zinazoendelea kujitokeza katika mchezo huo kinyume na sheria ambapo ameagiza TAKUKURU washirikishwe ili waweze kutoa elimu ya rushwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
  Amefafanua kuwa, iwapo vitendo vya rushwa havitadhibitiwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu, mchezo huo hautakuwa na maendeleo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERIKALI YAAGIZA TFF IWAKUTANISHE MAREFA NA TAKUKURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top