• HABARI MPYA

  Friday, January 07, 2022

  STARTIMES WAJA NA KAMPENI MPYA AFCON

  KAMPUNI ya Startmies wazindua kampeni mpya ikiwemo michuano mikubwa ya AFCON wakishirikiana na 10 BET.                        
  Hafla maalum ya uzinduzi huo imefanyika jjana na kuzimduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi . 
  Katika hafla hiyo ambapo Abbas amezindua kampeni maalum ya #MARA100ZAIDI ya kampuni ya Star Times kupitia ving'amuzi vyake ambayo imesheheni vipindi na chaneli mbalimbali ndani yake za kuonesha kazi za sanaa, michezo na utamaduni.


  Akizungumza kwa niaba ya Wizara na Serikali kwa ujumla katika uzinduzi huo Dkt. Abbasi amewapongeza Star Times kwa kuazisha chaneli mpya maalum kwa ajili ya kuonesha maudhui kutoka Tanzania pekee iitwayo ST Bongo.
  Alisema mwaka huu 2022 Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara wamejipanga kufanya mambo mengi makubwa ikiwemo kutoa mirabaha kwa wasanii, kuimarisha Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni na kuwataka wadau kutimiza wajibu wao.
  Ameongeza kuwa wadau wa sanaa hatuna budi kumuombea Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan dua njema kwani ametenda makubwa katika sanaa na michezo mwaka 2021 ili azidi kuwatendea mema zaidi Watanzania na mengi zaidi katika tasnia za ubunifu na burudani.             
  Katika hafla hiyo ambapo Meneja Masoko wa Star times Davis Malisa, alisema kuwa Kampuni ya Startimes imepata nafasi ya kuonyesha  michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) ambapo mechi zote 52 zitaonyeshwa kupita Kituo cha TV3  zikitangazwa kwa lugha ya Kiswahili.                                                                Malisa alisema kuwa katika michuano hiyoinayofanyika Januari 9 nchini Cameroon, kutakuwa na wachambuzi watano ambapo baadhi ya hao ni wachezaji wa zamani wa Simba, Yanga na timu ya Taifa Taifa Stars.                                                          Wachambuzi hao ni Amri Kiembe , Ivo Mapunda na Mussa Hassan Mgosi Startimes wanashirikiliana na Kampuni ya kubet ya 10 BET.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STARTIMES WAJA NA KAMPENI MPYA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top