• HABARI MPYA

  Wednesday, January 05, 2022

  MABINGWA YANGA SC WATOA ONYO KOMBE LA MAPINDUZI


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Taifa Jang’ombe usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 
  Mabao ya Yanga SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Heritier Ebenezer Ma Olongi Makambo dakika ya 33 na kiungo mpya, Dennis Nkane dakika ya 53.
  Mapema katika mchezo uliotangulia wa Kundi C, mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC walishinda 2-0 dhidi ya Selem View katika mchezo wa Kundi C hapo hapo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wameanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Selem View katika mchezo wa Kundi C jioni ya leo Uwanja wa Amaan.
  Mabao ya Simba yamefungwa na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 25 na kiungo Mzambia, Rally Bwalya dakika ya 53.Mabao ya Simba yamefungwa na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 25 na kiungo Mzambia, Rally Bwalya dakika ya 53.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABINGWA YANGA SC WATOA ONYO KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top