• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 02, 2020

  MWENYEKITI YANGA SC AKABIDHIWA RASIMU YA MABADILIKO YA MFUMO WA UENDESHWAJI WA KLABU

  HAFLA ya makabidhiano ya rasimu ya awali ya mabadiliko ya uwendeshwaji wa klabu ya Yanga imefanyika leo hoteli ya Serena Jijini Dar e sSalaam.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mabadiliko ya Yanga SC, Wakili Alex Mgongolwa akiambatana na Meneja mradi huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM, Mhandisi Hersi Said ndio wamekabidhi Rasimu hiyo.
  Rasimu hiyo imepokelewa na Mwenyekiti wa klabu, Dkt. Mshindo Msolla akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji na Wajumbe wa Baraza la Wadhamini na Wazee. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWENYEKITI YANGA SC AKABIDHIWA RASIMU YA MABADILIKO YA MFUMO WA UENDESHWAJI WA KLABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top