• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 04, 2020

  KMC YAICHAPA DODOMA JIJI 1-0 UHURU NA KUPANDA HADI NAFASI YA TANO KWENYE MSIMAMO WA LIGI

  BAO pekee la Emmanuel Mvuyekure dakika ya 58 limeipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 12 na kusogea nafasi ya tano, ikizidiwa pointi mbili mbili na zote, Ruvu Shooting na mabingwa watetezi, Simba SC wanaofuatana nafasi ya nne na ya tatu.
  Yanga SC ndiyo inaongoza Ligi Kuu kwa sasa kwa pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 13, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 26 za mechi 13.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KMC YAICHAPA DODOMA JIJI 1-0 UHURU NA KUPANDA HADI NAFASI YA TANO KWENYE MSIMAMO WA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top