• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 06, 2020

  WAZIRI JUNIOR ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU MWEZI JULAI, MINZIRO KOCHA BORA

  Na mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga SC, Waziri Junior amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwezi Julai wakati akiwa na timu yake ya zamani, Mbao FC iliyoshuka Daraja.
  Waziri ametwaa tuzo hiyo ya mwezi wa mwisho wa msimu wa Ligi baada ya kuwashinda Peter Mapunda wa Mbeya City na Obrey Chirwa wa Azam FC alioingia nao fainali.
  Naye kocha wa Mbao FC ya Mwanza, Fred Felix Minziro amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Julai akiwashinda Amri Said wa Mbeya City na Aristica Cioaba wa Azam alioingia nao fainali.
  Minziro aliiongoza Mbao kushinda michezo mitano kati ya sita waliyocheza ndani ya mwezi Julai na kupata sare moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAZIRI JUNIOR ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU MWEZI JULAI, MINZIRO KOCHA BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top