• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 13, 2020

  IDD NADO NA KIPA BENEDICT HAULE WAONGEZA MIKATABA YA KUENDELEA KUPIGA KAZI AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa Azam FC, Iddi Suleiman 'Nado', leo Alhamisi ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia kwenye timu hiyo.
  Nyongeza hiyo ya mkataba inamfanya kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2022.
  Nado amekuwa na kiwango kizuri tokea asajiliwe na timu hii msimu uliopita, akifanikiwa kufunga mabao tisa kwenye mashindano yote, saba katika ligi na mawili (Kagame Cup 2019, Rwanda).
  Iddi Suleiman 'Nado' (kushoto) akiwa na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat' wakati wa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja Azam FC
  Kipa Benedict Haule (kushoto) akiwa na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat' wakati wa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja Azam FC

  Naye kipa Benedict Haule ataendelea kusalia kwenye kikosi cha Azam FC kwa mwaka 2022, baada ya kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja.
  Kipa huyo amekuwa ni sehemu ya nguzo muhimu ndani ya kikosi hicho msimu uliopita akidaka vema mechi 10 za mwisho za ligi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: IDD NADO NA KIPA BENEDICT HAULE WAONGEZA MIKATABA YA KUENDELEA KUPIGA KAZI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top