• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 13, 2019

  WAKALA MMOJA TU WA WACHEZAJI TANZANIA NDIYE ANAYETAMBULIKA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) inaendelea kuwakumbusha wale wote wenye nia ya kuwa Mawakala wa Wachezaji fomu bado zinapatikana.
  Fomu zinapatikana kwenye tovuti ya TFF www.tff.or.tz kwa ada ya dola 100.
  Baada ya kujaza fomu inayoambatana na taarifa zako kutoka Interpol utalipia ada ya dola 2000 kupitia akaunti ya Bank ambayo ipo kwenye fomu.
  Mpaka sasa ni kampuni moja pekee ya Sports Soccer Management ndio inatambulika kufanya shughuli za Uwakala.
  TFF inasisitiza yeyote ambaye hana leseni hatambuliki kama ni Wakala na rai yetu kwao ni kuhakikisha wanasajiliwa na kutambulika kihalali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAKALA MMOJA TU WA WACHEZAJI TANZANIA NDIYE ANAYETAMBULIKA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top