• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 14, 2019

  REAL MADRID YASHINDA 2-1 AJAX WAKIKATALIWA BAO AMSTERDAM

  Marco Asensio akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la ushindi dakika ya 87 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Ajax kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Johan Cruijff Arena mjini Amsterdam. Real Madrid walitangulia kwa bao la Karim Benzema dakika ya 60 akimalizia kazi nzuri ya Vinicius Junior, kabla ya Ajax kusawazisha kupitia kwa Hakim Ziyech dakika ya 74 akimalizia pasi ya David Neres na kupata bao la pili lililofungwa na Nicolas Tagliafico akitumia makosa ya kipa Thibaut Courtois, lakini bao likakataliwa baada ya refa Damir Skomina kupata msaada wa marudio ya picha za video (VAR) 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID YASHINDA 2-1 AJAX WAKIKATALIWA BAO AMSTERDAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top