• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 17, 2019

  ULIMWENGU AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO JS SAOURA IKISHINDA 2-0 LIGI YA ALGERIA

  Na Mwandishi Wetu, BECHAR
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu jana amefungua akaunti yake ya mabao katika klabu yake mpya, JS Saoura baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 82 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Tadjenanet kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Algeria Uwanja wa Agosti 20, 1955 mjini Bechar.
  Bao la pili lilifungwa na Rafik Boukbouka dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo, Saoura inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi na kupanda kwa nafasi moja hadi ya sita.
  Saoura watakuwa na mechi tatu zaidi za Ligi ya Algeria dhidi ya CA Bordj Bou Arreridj Februari 22 , USM Bel Abbes Februari 26 na MO Bejaia Machi 2, kabla ya kucheza mechi zake mbili za mwisho za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Thomas Ulimwengu (wa pili kulia) akifurahia na wenzake baada ya mechi ya jana mjini Bechar
  Wataanza kwa kuikaribisha Simba SC ya Tanzania Machi 9 Uwanja wa Agosti 20, 1955 mjini Bechar kabala ya kusafiri kuwafuata Al Ahly Machi 16.
  Mechi za kwanza na wapinzani wake hao wa Kundi D Ligi ya Mabingwa, Saoura ilifungwa 3-0 na Simba SC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kabla ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Ahly mjini Bechar.
  Kwa sasa Al Ahly ndiyo inaongoza Kundi D kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Simba SC pointi sita, JS Saoura pointi tano, wakati AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ina pointi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMWENGU AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO JS SAOURA IKISHINDA 2-0 LIGI YA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top