• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 15, 2019

  ATHANAS MDAMU ASAINI MIAKA MITATU KUJIUNGA NA KARIOBANGI SHARKS YA KENYA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Singida United, Athanasi Mdamu leo amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Kariobangi Sharks ya Kenya.
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba Mdamu amesaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo ya Kenya kwa ridhaa ya uongozi wao. 
  Sanga amesema kwamba Kariobangi Sharks imemsajili Mdamu baada ya kumuona kwenye michuano ya SportPesa Super Cup mwezi uliopita mjini Dar es Salaam na kuvutiwa na uwezo wake.
  Athanasi Mdamu amejiunga na Kariobangi Sharks ya Kenya kwa mkataba wa miaka mitatu 

  “Viongozi wa Sharks waliwasiliana na Klabu yetu na baadaye tukamruhusu mchezaji huyo aende akaongeze maarifa kwenye soka kwa manufaa yake na Taifa letu,”amesema Sanga.
  Sanga amesema huo ni mwendelezo wa programu ya Singida United kuwaruhusu wachezaji kwenda kucheza soka nje ya nchi pale tu wanapopata timu kama ambavyo mkataba wa timu na mchezaji unavyoeleza.
  “Huyu ni Athanas amekwenda Kenya, tunategemea mchezaji mwingine kuondoka siku za karibuni kwenda kucheza barani ulaya na taratibu zake zote zimeshakamilika,” ameongeza Sanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ATHANAS MDAMU ASAINI MIAKA MITATU KUJIUNGA NA KARIOBANGI SHARKS YA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top