• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 18, 2019

  MECHI YA WATANI YAINGIZA SH. MILIONI 342, YANGA YAAMBULIA MILIONI 165

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO namba 270 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Yanga SC na Simba SC uliochezwa Jumamosi ya Februari 16, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam umeingiza jumla ya Sh. 342,825,000.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba jumla ya watazamaji 41,266 waliingia katika mchezo huo ambao Simba SC ilishinda 1-0.
  Ndimbo amesema katika jukwaa la VIP A waliingia watazamaji 546 kwa kiingilio cha Shilingi 30,000 na kupatikana jumla ya Sh. 16,380,000, VIP B na C waliingia watazamaji 3,185 kwa kiingilio cha Sh. 20,000 ikapatikana jumla ya Sh. 63,700,000.
  Ndimbo amesema majukwaa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani waliingia watazamaji 37,535 kwa kiingilio cha Sh. 7,000 na zimepatikana jumla ya Sh. 262,745,000
  Amesema kwamba kutokana na mapato hayo, klabu ya Yanga iliyokuwa mwenyeji wa mchezo huo imepata Sh. 165, 215,792.86, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamepata Sh. 52,295,338.98 kutokana na Kodi (VAT) na wasimamizi wa mapato, kampuni ya Selcom imepata Sh. 15,170,006.25.
  Fedha nyingine, TFF wamepata Sh. 13,767,982.74, Uwanja Sh. 41,303,948.22, Gharama za mchezo Sh. 19,275,175.83, Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) Sh. 24,782,368.93, Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Sh. 2,753,596.55 na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) Sh. 8,260,789.64. 
  MGAWANYO WA MAPATO MECHI YA WATANI 
  VAT                             52,295,338.98
  Selcom                       15,170,006.25
  TFF                              13,767,982.74
  Uwanja                        41,303,948.22
  Young Africans         165,215,792.86
  Gharama za mchezo  19,275,175.83
  TPLB                          24,782,368.93
  BMT                           2,753,596.55
  DRFA                          8,260,789.64
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI YA WATANI YAINGIZA SH. MILIONI 342, YANGA YAAMBULIA MILIONI 165 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top