• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 21, 2019

  MSHAMBULIAJI MDENMARK MWENYE ASILI YA TANZANIA, YUSUF POULSEN AJA NCHINI

  Na Grace Semfuko-MAELEZO
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Denmark, Yussuf Yurary Poulsen mwenye asili ya Tanzania anatarajiwa kuzuru nchini kwa shughuli za kiutalii.
  Mchezaji wa klabu ya RB Leipzig ya Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga analetwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na taasisi ya Magnet Youth Sports Organization of Tanzania (MYSOT).
  Na mpango huo umekuja baada ya TTB na taasisi hiyo kushirikiana kuandaa safari ya kitalii ya kocha Andreas Pach na Martin Hammel wa Ujerumani ya kupanda Mlima Kilimanjaro Februari 15 hadi 19 mwaka huu na kutembelea vivutio vya Utalii lengo likiwa ni kuutangaza Utalii wa Tanzania.  Mshambuliaji wa RB Leipzig, Yussuf Poulsen anatarajiwa kuzuru nchini Tanzania kwa shughuli za kiutalii

  Andreas Pach na Mwenzake Martin Hammel ni Makocha ambao wapo nchini Tanzania wakitokea kwenye mradi wa ITK Pathfinder 2019 uliopo chini ya Chuo Kikuu cha Leipzig cha nchini Ujerumani  mradi ambao unalenga kuwafundisha Makocha na Vijana kwenye mchezo wa Soka na kumtangaza Mchezaji nyota mwenye asili ya Tanzania anaechezea Ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani Yusuph Poulsen.
  Wakiwa Nchini Tanzania Makocha hao walipata nafasi ya kutoa mafunzo ya michezo kwa makocha 25 na Vijana 120 wa Kitanzania lengo likiwa ni kukuza Vipaji vya michezo  nchini.
  Ujio wa makocha hao ni mwaliko wa Magnet Youth Sports Organization chini ya Mkurugenzi mwendeshaji wake Tuntufye Mwambusi  ambapo bodi ya utalii kupitia ujio huo wameamua kushirikiana katika kuutangaza utalii wa ndani ikiwepo Mlima Kilimanjaro 
  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema bodi hiyo imeanza mazungumzo ya wali na mchezaji huyo nyota Yusuph Poulsen ambaye anachezea ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani ili kuutangaza Utalii wa ndani.
  “kwetu sisi TTB tunachukulia ujio huu wa makocha hawa na mashirikiano yaliyopo kati ya ITK na Tanzania, na tumeanza mazungumzo na Mchezaji mwenye asili ya Tanzania Bw. Yusuph Poulsen ikiwa ni mkakati wetu wa kutumia watu maarufu katika kuutangaza utalii wa ndani na tunataka kumfanya kuwa  Balozi wa hiyari wa utalii wa Nchi yetu” alisema Jaji Mstaafu Thomas Mihayo.
  Nae mmoja kati ya makocha hao wawili wa kutoka Nchini Ujerumani Bw.Andreas Pach alisema Tanzania kuna Vipaji vingi vya Michezo na hivyo ni muhimu kuviendeleza.
  “tumefurahishwa kuona Watanzania ni watu wakarimu, Tanzania kuna Vijapi vingi vya Michezo na vipaji hivi vikiendelezwa tutakuwa mbali kimichezo, Poulsen anafanya Vizuri sana kule Ujerumani” alisema Andreas Pach
  Kwa upande wake Mkurugenzi mwendeshaji wa Magnet Youth Sports Organization Bw. Tuntufye Mwambusi alisema wataendelea kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania na wanamichezo katika kukuza Utalii wa Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI MDENMARK MWENYE ASILI YA TANZANIA, YUSUF POULSEN AJA NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top