• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 15, 2019

  MBAO YAZINDUKA YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0, NDANDA YAIPIGA ALLIANCE 1-0 PIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mbao FC imezinduka leo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Kwa ushindi huo uliotokana nao bao pekee la Raphael Siame dakika ya 33, unaifanya Mbao FC ifikishe pointi 36 baada ya kucheza mechi 26 na kupanda hadi nafasi ya sita kutoka ya saba, huku Ruvu Shooting ikibaki nafasi ya 13 na pointi zake 30 za mechi 27.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Ndanda FC imeshinda 1-0 dhidi ya Alliance FC ya Mwanza Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, bao pekee la Ismail Mussa dakika ya 17, wakati KMC FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

  Nayo Mbeya City imelazimshwa sare ya kufungana bao 1-1 na Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. John Kabanda alianza kuifungia Mbeya City dakika ya 54, kabla ya Jacob Massawe kuisawazishia Stand United dakika ya 86.
  Ndanda FC inasogea nafasi ya 17 ikifikisha pointi 29 katika mechi ya 25, Mbeya City inabaki nafasi ya 10 licha ya kufikisha pointi 30 katika mechi 24, Stand United inabaki nafasi ya 12 licha ya kufikisha pointi 30 katika mechi ya 27 na Alliance FC inabaki nafasi ya nane na pointi zake 33 baada ya kucheza mechi 27.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mabingwa watetezi, Simba SC kumenyana na mahasimu wao wa jadi, Yanga SC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, wakati Jumapili Lipuli FC wataikaribisha Singida United Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBAO YAZINDUKA YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0, NDANDA YAIPIGA ALLIANCE 1-0 PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top