• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 28, 2019

  IDDI NADO APIGA BAO LA KUOMBEA RADHI MBEYA CITY BAADA YA ‘KUWATOA’ KOMBE LA TFF

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  MSHAMABULIAJI chipukizi nchini, Iddi Suleiman ‘Naldo’ jana alifunga bao pekee dakika ya 55, timu yake Mbeya City ikiichapa 1-0 Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokine mjini Mbeya.
  Bao hilo lilipokewa kama la kuombea radhi kwa mchezaji huyo baada ya kukosa penalti ya mwisho Mbeya City ikitolewa na African Lyon katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) wiki iliyopita.
  Mbeya City ilitolewa na African Lyon kwa penalti 4-3 kuduatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la TFF mjini Dar es Salaam baada ya Iddi ‘Naldo’ kukosa penalty ya mwisho.

  Iddi Suleiman ‘Naldo’ jana ameifungia bao pekee Mbeya City ikiichapa 1-0 Singida United 

  Lakini baada ya ushindi wa jana, Mbeya City imefikisha pointi 33 baada ya kucheza mechi 26 na kujiinua kutoka nafasi ya 17 hadi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu yenye timu 20, wakati Singida United inabaki nafasi ya 18 kwa pointi zake 29 za mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: IDDI NADO APIGA BAO LA KUOMBEA RADHI MBEYA CITY BAADA YA ‘KUWATOA’ KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top