• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 16, 2019

  SIMBA NA YANGA WAPANGIANA VIKOSI VYA KUSHAMBULIANA ‘MWANZO MWISHO’

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mbelgiji wa Simba SC, Patrick Aussems amewaanzisha pamoja washambuliaji wake, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Nahodha John Bocco katika mchezo dhidi ya mahasimu, Yanga SC jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
  Kwa mahasimu wao wa jadi, Yanga SC naye kocha Mwinyi Zahera kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amewapanga pamoja washambuliaji wake watatu, Heritier Makambo, Amissi Tambwe na Ibrahim Ajib.
  Safu zote za ushambuliaji zitakuwa na wachezaji wawili wa kigeni na mzawa mmoja; Simba Mganda Okwi na Mnyarwanda Kagere wakicheza na Bocco wakati Yanga Mkongo Makambo na Mrundi Tambwe wakicheza na Ajibu.
  Ibrahim Ajibu (kulia) na John Bocco (kushoto) wazawa pekee wanaoanza kwenye safu za ushambuliaji Simba na Yanga leo

    
  Kwa ujumla, Aussems amerudia kikosi kile kile kilichoifunga Al Ahly 1-0 katikati ya wiki katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Jumanne wiki hii hapo hapo Uwanja wa Taifa na Zahera amerudia kikosi kilichoshinda mechi iliyopita ya Ligi Kuu 1-0 dhidi ya JKT Tanzania.
  Kwa tathimini ya haraka haraka timu zote zimepanga vikosi vya kucheza mfumo wa kushambulia zaidi, wote wakitumia watu watatu katika kushambulia na viungo watatu.
  Kwa ujumla kikosi cha Simba SC kinachoanza leo ni; Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Serge Wawa, James Kotei, Clatous Chama, Jonas Mkude, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.
  Katika benchi wapo Deo Munishi ‘Dida’, Nicholas Gyan, Yussuf Mlipili, Muzamil Yassin, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga na Rashid Juma.
  Bechi la Ufundi; ni Kocha Mkuu, Patrick Aussems, Msaidizi Dennis Kitambi, Kocha wa mazoezi ya viungo, Mtunisia Adel Zrane, Kocha wa Makipa Muharami Mohammed, Meneja Patrick Rweyemamu, Mtunza Vifaa Hamisi Mtambo na Daktari Yassin Gembe. 
  Yanga SC; Ramadhani Kabwili, Paulo Godfrey ‘Boxer’, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Papy Kabamba Tshishimbi, Heritier Makambo, Amissi Tambwe na Ibrahim Ajibu.
  Benchi; Klaus Kindoki, Juma Abdul, Said Juma ‘Makapu’, Haruna Moshi ‘Boban’, Mohammed Issa ‘Banka’, Mrisho Ngassa na Matheo Anthony. 
  Benchi la Ufundi ni Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera, Msaidizi Noel Mwandila, Kocha wa Makipa Juma Pondamali, Meneja Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mratibu Hafidh Saleh, Daktari Edward Bavu na Mtunza Vifaa, Mohammed Omar ‘Mpogolo’.
  Mechi hiyo itakayochezeshwa na na refa Hans Mabena atakayesaidiwa na washika vibendera Mohammed Mkono, wote wa Tanga na Kassim Mpanga, wakati Heri Sasi atakuwa refa wa akiba wote wa Dar es Salaam, itaanza Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa ikionyeshwa moja kwa moja na chaneli ya Azam Sports 2 ya Azam TV.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA WAPANGIANA VIKOSI VYA KUSHAMBULIANA ‘MWANZO MWISHO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top