• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 14, 2019

  SAMATTA 'ALAMBWA' KADI GENK IKITOA SARE UGENINI EUROPA LEAGUE

  Na Mwandidhi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku huu ameonyeshwa kadi ya njano, timu yake KRC Genk ikilazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, Slavia Prague Uwanja wa Sinobo mjini Praha, Jamhuri ya Czech katika mchezo wa kwanza hatua ya 32 Bora UEFA Europa League.
  Samatta alionyeshwa kadi hiyo dakika ya 89 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua Genk wakipigana kwa uwezo wao wote kushinda ugenini bila mafanikio.
  Sasa Genk wanahamishia vita nyumbani kwao wakitarajiwa kuwakaribisha Slavia Prague Februari 21 Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.

  Mbwana Samatta akimtoka beki wa Slavia Prague leo Uwanja wa Sinobo mjini Praha 

  Kwa Samatta mwenye umri wa miaka 26, leo amefikisha mechi 23 za Europa League kuichezea Genk tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 14.
  Kwa ujumla Samatta ameichezea Genk mechi 142 za mashindano yote na kuifungia mabao 58, mengine 43 amefunga kwenye mechi 109 za Ligi na mawili kwenye tisa za Kombe la Ubelgiji
  Kikosi cha Slavia Prague kilikuwa; Kolar, Coufal, Zmrhal/Olayinka dk61, Husbauer/Kral dk77, Ngadeu, Kudela, Stoch, Boril, Skoda/van Buren dk76, Soucek and Sevcik.
  KRC Genk; Vukovic, Maehle, Aidoo, Dewaest, De Norre, Heynen, Malinovskyi, Fiolic/Pozuelo dk57, Ndongala/Paintsil dk69, Trossard/Piotrowski dk87 na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA 'ALAMBWA' KADI GENK IKITOA SARE UGENINI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top