• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 24, 2019

  MSUVA AFUNGA MABAO MAWILI DIFAA HASSAN EL JADIDI YASHINDA 2-0 LIGI YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana amefunga mabao yote mawili, klabu yake Difaa Hassan El - Jadida ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Ittihad Tanger.
  Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Morocco uliofanyika Uwanja wa Grand Stade de Tanger mjini Tanger, Msuva alifunga mabao yake dakika ya kwanza na 29.
  Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El – Jadida inafikisha pointi 24 baada ya kucheza mechi 19 na kujiinua kwa nafasi mbili kwenye msimamo wa Botola hadi ya tisa.
  Simon Msuva usiku wa jana amefunga mabao yote mawili, Difaa Hassan El - Jadida ikishinda 2-0 dhidi ya Ittihad Tanger

  Difaa Hassan El – Jadida sasa inazidiwa pointi tatu na Ittihad Tanger iliyo nafasi tatu kwenye msimamo wa Botola baada ya kucheza mechi 19 pia, nyuma ya Raja Casablanca yenye pointi 28 za mechi 16 na Wydad Casablanca yenye pointi 39 za mechi 18.
  Lakini Difaa Hassan El – Jadida pia inaizidi pointi saba tu, Kawkab Marrakech inayoshika mkia kwenye Ligi Kuu ya Morocco baada ya kucheza mechi 19, ikiwa nyuma ya Rapide Oued Zem na Chabab Rif Hoceima zenye pointi 19 kila moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVA AFUNGA MABAO MAWILI DIFAA HASSAN EL JADIDI YASHINDA 2-0 LIGI YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top