• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 13, 2019

  ARSENAL UGENINI KWA WATENGENEZA MAGARI BATE BORISOV

  PENGINE ulikuwa hujui jina BATE ni kifupisho cha Borisov Automobiles and Tractor Electronics, ndio! Nimetaja trekta, FC BATE inamilikiwa na kiwanda cha magari huko nchini Belarus. FC BATE wameshinda taji la Ubingwa wa ligi kuu ya Belarus mara 13 mfululizo, hawa ndio watawakaribisha Arsenal katika uwanja wa Borisov Arena Alhamisi hii majira ya saa 2:55 Usiku.
  Mchezo wa Arsenal ni moja kati ya 16 itakayochezwa Usiku wa Alhamisi hii katika hatua ya 32 bora. Michezo ambayo kwa hapa Tanzania itarushwa na kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee kupitia chaneli zao za michezo.
  Kwa upande wao Arsenal huenda wakaendelea kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Americk Aubameyang ambaye ni mgonjwa. Hata hivyo Arsenal watajipa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo baada ya kushinda mchezo wa ugenini dhidi ya Huddersfield 2-1 katika ligi kuu ya Uingereza. Itakumbukwa pia msimu uliopita Arsenal waliichapa BATE 4-2 ugenini na kisha 6-0 katika dimba la Emirates, hivyo wataingia uwanjani historia ikiwabeba.
  Kwa upande wa Chelsea wao watahitaji kuwa na utimamu wa kimchezo baada ya kufungwa ugenini kwa Manchester City kwa magoli 6-0 Jumapili iliyopita. Chelsea pia watakuwa ugenini nchini Sweden kucheza dhidi ya Malmo FF. Malmo imewahi kushinda mara moja tu dhidi ya timu za Uingereza. Mechi hii itaruka LIVE majira ya saa 5:00 Usiku kupitia ST World Football pekee.
  Michezo mingine itayakayochezwa Alhamisi Usiku Saa 2:55 ni SS Lazio vs Sevilla (Sports Premium), Krasnodar vs Leverkusen (Sports Arena) na ile ya Saa 5:00 Usiku ni Sporting CP vs Villarreal (Sports Focus), Celtic FC vs Valencia CF (Sports Arena), FC Zurich vs Napoli SSC (Sports Premium) na nyingine zote kupitia chaneli za michezo sa StarTimes.
  Michezo yote ya Europa league inaonekana kupitia StarTimes ambapo mteja anatakiwa kulipia kifurushi cha kati, kwa upande wa Antenna ni MAMBO Tsh 14,000 pekee na kwa upande wa dish ni SMART kwa Tsh 21,000 pekee. Pia mechi za Arsenal na Chelsea zina uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili.
  Kuhusu Star Media (T) Ltd;
  StarTimes ni kampuni ya Matangazo ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia zaidi ya wateja milioni 10 katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa la maudhui lenye chaneli 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu, tamthiliya, michezo, burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na vingine vingi. Matazamio ya Kampuni ni “Kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata, inamudu, inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa Televisheni ya kidigitali”

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL UGENINI KWA WATENGENEZA MAGARI BATE BORISOV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top