• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 28, 2019

  TIBAR JOHN WA SINGIDA UNITED AENDA ULAYA KUJIUNGA NA TIMU YA JAMHURI YA CZECH

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, John Tibar George jana ameondoka nchini kwenda kujiunga na klabu ya MFK FC ya Jamhuri ya Czech.
  Mchezaji huyo wa Singida United, Tibar aliondoka Saa 5:00 usiku wa jana akipitia Ufaransa ambako atakaa kwa muda usiopungua wiki moja kwenye klabu Toulouse FC kwa ajili ya mazoezi maalum ya kumuweka fiti na kumuongeza maarifa ya kioska.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United FC, Festo Richard Sanga alisema jana kwamba vibali vyote vimekwishatumwa kwenye klabu yake mpya ikiwa ni pamoja na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
  John Tibar George jana amekwenda kujiunga na MFK FC ya Jamhuri ya Czech

  “Hivyo anakwenda huko kuanza maisha ya soka moja kwa moja. Tunashukuru sana wote waliohusika kufanikisha hili, zaidi TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kwa ushirikiano wao wote katika kipindi chote cha kuhakikisha vibali vya mchezaji huyu vinapatikana kwa wakati,”alisema Sanga Festo.
  Mkurugenzi huyo amesema kwamba huo ni mwendelezo wa Singida United kuwafungulia njia wachezaji wa Kitanzania kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na wataendelea kufanya hivyo kwa maslahi ya klabu, timu ya taifa na wachezaji wenyewe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIBAR JOHN WA SINGIDA UNITED AENDA ULAYA KUJIUNGA NA TIMU YA JAMHURI YA CZECH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top