• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 17, 2019

  LIPULI FC YASAWAZISHA DAKIKA YA MWSHO KUPATA SARE NA SINGIDA UNITED 2-2

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  TIMU ya Lipuli FC leo imenusurika kuchapwa nyumbani baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Na aliyeinusuru Lipuli FC inayofundishwa na kocha Suleiman Matola leo amekuwa ni mshambuliaji Miraj Athumani Madenge aliyefunga bao la kusawazisha dakika ya 90 na ushei.
  Ulikuwa ni mchezo wa funga nikifunge, baada ya Singida United inayofundishwa na kocha Mserbia, Dragan Popadic kutangulia kwa bao la winga Geoffrey Mwashiuya dakika ya 46, kabla ya Haruna Shamte kuisawazishia Lipuli FC dakika ya 61.

  Boniphace Maganga akaifungia Singida United bao la pili dakika ya 84, kabla ya mchezaji mwenzake wa zamani wa timu ya vijana ya Simba SC, Miraj Athumani ‘Madenge’ au Shevchenko kusawazisha Lipuli dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, Lipuli inajiongezea pointi moja na kufikisha 38 baada ya kucheza mechi 26 na kupanda hadi nafasi ya nne kutoka ya tano, ikiishusha KMC yenye pointi 37 za mechi 26 pia, wakati Singida United inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 24 na kupanda hadi nafasi ya 15 kutoka ya 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIPULI FC YASAWAZISHA DAKIKA YA MWSHO KUPATA SARE NA SINGIDA UNITED 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top