• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 27, 2019

  KICHUYA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA 10 ENNPI YACHAPWA 3-1 SASA INASHIKA MKIA MISRI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Shizza Ramadhani Kichuya jana ametokea benchi dakika 10 za mwisho timu yake, ENPPI ikichapwa mabao 3-1 na Al Masry katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri uliofanyika Uwanja wa Jeshi la nchi hiyo mjini Suez.
  Kichuya aliyejiunga na ENPPI mwezi huu kwa mkopo kutoka Pharco FC ya Daraja la Kwanza iliyomsajili kutoka Simba SC ya Dar es Salaam Januari mwaka huu, aliingia dakika ya 80 kwenda kuchukua nafasi ya Emad Fathy wakati huo tayari timu yake hiyo iko nyuma kwa mabao 2-1.
  Na ni Emad Fathy ndiye aliyefunga bao la ENPPI dakika ya 47, ambalo lilikuwa la kusawazisha kufuatia Mahmoud Wadi kutangulia kuifngia Al Masry dakika ya 13, kabla ya mshambuliaji Mnigeria, Austin Amutu kuwafungia wenyeji bao la pili dakika ya 74.

  Shizza Kichuya (kulia) jana ametokea benchi ENPPI ikichapwa 3-1 na Al Masry katika Ligi Kuu ya Misri 

  Na akiwa uwanjani, Kichuya aliyejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro akashuuhudia ENPPI iliyomaliza pungufu baada ya kipa wake, Amr Hossam kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 82 ikipachikwa bao la tatu, mfungaji Islam Issa dakika ya 84.
  Mchezaji mwingine wa Tanzania, Yahya Zayd jana hakuwepo hata benchi timu yake, Ismailia ikilazimishwa sare ya 0-0 na El Geish katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Misri.
  Baada ya matokeo ya jana, ENPPI sasa inashika kwenye Ligi Kuu ya Misri inayoshirikisha timu 18 ikibaki na pointi zake 21 baada ya kucheza mechi 23, wakati Ismailia imefikisha pointi 28 katika mchezo wa 20 ingawa inabaki katika nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KICHUYA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA 10 ENNPI YACHAPWA 3-1 SASA INASHIKA MKIA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top