• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 14, 2019

  KESSY AISAIDIA NKANA FC KUIPIGA AL HILAL 2-1 KITWE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, KITWE
  BEKI Mtanzania, Hassan Ramadhani Kessy jana ameisaidia timu yake, Nkana FC kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Al Hilal Omdurman katika mchezo wa Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Nkana mjini Kitwe nchini Zambia.
  Haukuwa ushindi mwepesi, kwani Nkana FC pamoja na kuwa nyumbani walilazimika kutoka nyuma baada ya kutanguliwa kwa bao la dakika ya saba la Waleed Bakhet Hamid aliyemalizia kazi nzuri ya mshambuliaji mwenza kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Ilunga Mbombo.
  Alianza Freddy Tshimenga kuisawazishia Nkana FC dakika ya 14, akimalizia pasi ya Ronald Kampamba kabla ya Walter Bwalya kufunga bao la ushindi dakika ya 75, akimalizia pasi ya Simon Bwalya.

  Hassan Kessy jana ameisaidia Nkana FC kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Al Hilal Omdurman

  Sasa kila timu katika Kundi C ina pointi tatu baada ya mechi mbili za kwanza, huku Nkana FC ikishika mia kutokana na wastani wake mdogo wa mabao, ndugu zao ZESCO United wakiongoza wakifuatiwa na Al Hilal na Asante Kotoko.
  Mechi zijazo, Nkana watawakaribisha Asante Kotoko Jumapili ya Februari 24 kuaniza Saa 10:00 jioni na ZESCO United watakuwa wenyeji wa Al Hilal kuanzia Saa 1:00 usiku.
  Kikosi cha Nkana FC kilikuwa; K. Malunga, J. Musonda, M. Mohammed, A. Bahn, H. Kessy, S. Malambo, H. Chisala/, K. Kampamba/, F. Tshimenga, R. Kampamba/ na W. Bwalya.
  Al Hilal;  J. Salim, Faris Abdalla Mamoun, Samawal Merghani, E. Ariwachukwu, Abdellatif Boya, B. Diarra, Sharaf Eldin Ali/, Moumen Esam/, Mohamed Mokhtar, I. Mbombo na Waleed Bakhet Hamid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KESSY AISAIDIA NKANA FC KUIPIGA AL HILAL 2-1 KITWE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top