• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 18, 2019

  SERENGETI BOYS WAINGIA KAMBINI ARUSHA KUJIANDAA NA MICHUANO YA AFCON U17

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imepiga Kambi Jijini Arusha kujiandaa na Fainali za Afrika za Vijana U17 zitakazofanyika Tanzania mwezi Aprili.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba kwa sasa Serengeti Boys inaendelea na maandalizi katika Uwanja wa Aghakhan mazoezi yakifanyika asubuhi na jioni.
  Itarudi Dar es salaam mwishoni mwa mwezi Februari kabla ya kuondoka Machi 1,2019 kueleka nchini Uturuki kwenye mashindano ya UEFA ASSIST yanayoshirikisha timu 8 za Afrika na timu 4 za Ulaya zilizogawanywa kwenye makundi 3.

  Wachezi 31 wapo Kambini Jijini Arusha wakiendelea na mazoezi hayo kujiandaa na AFCON U17 itakayofanyika Tanzania.
  Tayari nembo ya mashindano hayo imezinduliwa wakati vikao mbalimbali vya Kamati ya maandalizi vikiendelea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS WAINGIA KAMBINI ARUSHA KUJIANDAA NA MICHUANO YA AFCON U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top