• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 13, 2019

  SINGIDA UNITED YATINGA 16 BORA KOMBE LA TFF BAADA YA KUIPIGA JKT 1-0 NAMFUA

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  TIMU ya Singida United imefanikiwa kuingia hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Namfua mjini Singida.
  Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, Kenny Ally Mwambungu kwa shuti la umbali wa mita 45, akiiwezesha SIngida United kuitoa JKT Tanzania kwa mara ya pili mfululizo kwenye michuano hiyo.   
  Singida United inayofundishwa na kocha Mserbia, Dragan Popadic sasa itamenyana na Coastal Union ya Tanga katika hatuaya 16 Bora kati ya Februari 22 na 25, mwaka huu, kwa mara nyingine wakiwa nyumbani Uwanja wa Namfua. 

  Mechi nyingine za hatua ya 16 Bora ni Yanga SC na Namungo FC Uwanja wa Taifa, KMC na mabingwa watetezi Mtibwa Sugar, African Lyon na Mbeya City FC Uwanja wa Uhuru, Azam FC na Rhino Rangers Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Alliance FC na Dar City Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza, Lipuli FC na Dodoma FC Uwanja wa Samora mjini Iringa na Boma FC na Kagera Sugar mjini Mbeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YATINGA 16 BORA KOMBE LA TFF BAADA YA KUIPIGA JKT 1-0 NAMFUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top