BONDIA Muingereza Anthony Joshua amemuonya Deontay Wilder kuacha 'kupayuka' kwenye mitandao na vyombo vya habari, kama anataka kupigana naye afate taratibu.
Joshua amemuambia Wilder pambano litafanikiwa iwapo wao watatimiza masharti yake kwa kupeleka ofa yao kwa Meneja waje, Eddie Hearn kwa ajili ya pambano la ubingwa wa WBC uzito wa juu.
Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 28, Joshua, ambaye alimtwanga Carlos Takam kwa Technical Knockout (TKO) na kutetea mikandsa yake ya ubingwa wa dunia uzito wa juu, amesistiza mpinzani kweli ni yule anayefuata taratibu katika kuomba pambano.
Anthony Joshua amemuambia Mmarekani, Deontay Wilder atoe ofa ya pambano, badala ya kuendelea kuseam pembeni PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Hivi karibuni, Wilder amemshutumu promota wa Joshua, Hearn kwa kuchelewesha majadiliano ya pambano hilo na bingwa wa WBO, Joseph Parker anamchukulia yeye kama chaguoa sahihi.
Kabla ya Wilder kumsimamisha Bermane Stiverne ndani ya raundi moja katika pambano lake la sita la kutetea taji lake la WBC uzito wa juu, Hearn alizungumzia mpango wa kumpa ofa ya kupigana na mpinzani wa Joshua, Dillian Whyte.
Pamoja na hayo, Joshua alisema: "Kama Wilder hatatoa ofa, tutafanya hii kwa vipengele vyetu. Wamlete na ofa yake, na tuone wanajifikiria nini kwenye hiyo ofa. Hiyo inakwenda kwa bingwa tu, Deontay Wilder na Joseph Parker. Wote wako sawa baina yao,".
"Hakuna tatizo kama Wilder anataka kupigana mapema mwakani, lakini hakuna ofa iliyotolewa. Kila mmoja anasema anataka kupigana, na kisha amekaa huko kunisubiri mimi ndiyo niliofanyie kazi hilo,"
"Tunachotakiwa kufanya - ambacho Eddie anafanya- amekwenda Marekani kuweka muda. Hakuna ofa iliyotolewa, kwa upande wao, au wetu; tuna uwezo wa kuchagua eneo (la kupigania), na sasa tunapoteza muda na juhudi kuzungusha mpira," amesema.
0 comments:
Post a Comment