![]() |
Mbwana Samatta akimtoka mchezaji wa USM Alger |
Samatta alifunga bao hilo dakika ya 79 kwa penalti baada yeye mwenyewe kuangushwa, ambalo lilikuwa la pili kwa Mazembe baada ya Rainford Kalaba kufunga la kwanza dakika ya 27, kabla ya USM kupata la kufutia machozi dakika ya 88 kupitia kwa Mohamed Seguer.
Mazembe sasa itahitaji hata sare katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Lubumbashi ili kutwaa taji la tano la ubingwa wa Afrika.
Samatta alitolewa dakika ya 86 kumpisha Roger Assale dakika ya 86, wakati Adjei Nii aliihukua nafasi ya Mtanzania mwingine wa Mazembe, Thomas Ulimwengu dakika ya 90 na ushei.
0 comments:
Post a Comment