• HABARI MPYA

    Wednesday, September 02, 2015

    KIMEELEWEKA, TWIGA STARS SASA KUONDOKA KESHO KWENDA KONGO-BRAZZAVILE

    Na Genofeva Matemu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Taifa ya Tanzania yenye wachezaji wapatao 30 na viongozi 7 wa michezo mbalimbali inatarajia kuondoka Jijiji Dar es Salaam kesho jioni na ndege maalum kuelekea Congo Brazaville kushiriki katika Michezo ya Afrika (All Africa Games) itakayofunguliwa rasmi Septemba 4, 2015.
    Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari kuhusu Timu ya Taifa itakayoshiriki katika Michezo ya Afrika (All Africa Games) huko Congo Brazzaville.

    Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Michezo, Juliana Yassoda (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Timu ya Taifa itakayoshiriki katika Michezo ya Afrika (All Africa Games) Congo Brazaville. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene

    Mwambene amesema kuwa Tanzania itawakilishwa na Michezo sita ikiwemo Mchezo wa Ngumi za Ridhaa yenye wachezaji watatu, Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake (Twiga Stars) yenye wachezaji 18, na Timu ya Riadha yenye wachezaji wanne.
    Nyingine ni Timu ya kuogelea yenye wachezaji wawili, wachezaji wawili wa Judo pamoja na Michezo kwa watu wenye Ulemavu yenye wachezaji wawili.
    Naye Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Michezo, Juliana Yassoda amesema kuwa Timu ya Taifa ya Tanzania ilikua iondoke kwenda Congo Brazzaville leo lakini kutokana na ugumu wa upatikanaji wa nafasi katika ndege mbalimbali timu hiyo imelazimika kuondoka kesho na usafiri maalum.
    Michezo ya Afrika (All Africa Games) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho na Twiga Stars itafungua dimba na Ivory Coast Septemba 6, kabla ya kumenyana na Nigeria Septemba 9 na kumaliza mechi za kundi lake kwa kumenyana na wenyeji Kongo-Brazzavile Septemba 12.
    Timu mbili kutoka kundi A zitaungana na timu mbili nyingine kutoka kundi B kucheza hatua ya nusu fainali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIMEELEWEKA, TWIGA STARS SASA KUONDOKA KESHO KWENDA KONGO-BRAZZAVILE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top