Na Princess Asia, JOHANNESBURG
KOCHA Mzungu anawanoa makipa wa Simba SC katika kambi yao, Afrika Kusini wakati kocha wa makipa wa Oman, Choke Abeid anatarajiwa kutua wakati wowote kuanza rasmi kazi ya ‘kuwafua’ makipa wa timu hiyo, baada ya kutupiwa virago kwa Iddi Pazi ‘Father’.
Pazi aliachwa Dar es Salaam wakati Simba SC inaondoka jana na ingawa hajaambiwa chochote, lakini ndiyo ametimuliwa- baada ya uongozi kuamini viwango vya makipa wao vimeshuka chini yake.
Simba SC imeanza mazoezi leo kwenye viwanja vya
Hoteli ya Eden Vale Petra mjini Johannesburg walipofikia na keshokutwa watacheza mchezo wa kirafiki na wenyeji Orlando Pirates mjini Johannesburg.
Simba ipo Afrika Kusini tangu jana kwa ajili ya maandalizi yake ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 18, mwaka huu Dar e Salaam.
Suleiman Matola aliyekuwa kocha Msaidizi tangu wakati wa Mcroatia, Zdravko Logarusic anaendelea kuwa Msaidizi wa Mzambia, Patrick Phiri wakati Meneja anaendelea Nico Nyagawa.
Katika mchezo na Pirates, Simba SC itawakosa wachezaji wake walio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda, The Cranes- ambao wanatarajiwa kujiunga na wenao kuanzia Jumatatu.
Hata hivyo, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na The Cranes yeye hatakwenda kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati ya wiki.
Wachezaji wa Simba SC walioko Stars ni; mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu.
Simba SC itakuwa ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani.
Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18.

![]() |
| Kocha Mzungu akiwanoa makipa wa Simba SC leo Johannesburg |

| Mzungu akiwanoa makipa wa Simba leo |
![]() |
| Simba SC wakijifua Afrika Kusini leo |

.png)
0 comments:
Post a Comment