• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 25, 2014

  YANGA SC YAICHAPA STAND UNITED 3-0, TEGETE ATOKEA BENCHI NA KUPIGA MBILI

  YANGA SC imeibwaga Stand United mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Ushindi huo unaifanya Yanga SC itimize pointi 10 baada ya mechi tano na sasa inakabana na Azam FC na Mtibwa Sugar kileleni.
  Yanga SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao 1-0, lililofungwa na Genilson Santana Santos ‘Jaja’ dakika ya 13 baada ya kupokea pasi ya Mbrazil mwenzake, Andrey Coutinho.
  Kipindi cha pili, mshambuliaji Jerry Tegete aliyetokea benchi aliifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 78 baada ya kupata pasi ya Hussein Javu, aliyetokea benchi pia.
  Tegete tena aliingia Yanga SC bao la tatu dakika ya 89 na baada ya mashabiki walimbeba juu kwa kuchangia ushindi huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA STAND UNITED 3-0, TEGETE ATOKEA BENCHI NA KUPIGA MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top