• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 29, 2014

  RONALDO AMGARAGAZA 'VIBAYA' MESSI TUZO ZA LA LIGA

  NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa tena tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kumpiku mpinzani wake, Lionel Messi katika tuzo za Ligi ya Hispania.
  Mshambuliaji huyo wa Real Madrid ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa La Liga usiku wa Jumatatu baada ya kuwafungia mabao 31 katika ligi mabingwa hao wa Ulaya.
  Hilo linaweza kuwa pigo kwa Messi, ambaye alitwaa kila tuzo miaka mitano iliyotangulia. 
  Cristiano Ronaldo (kushoto), akiwa na mpenzi wake Irina Shayk wakati wa kupokea tuzo hizo

  TUZO ZA LIGA 

  Mchezaji Bora: Cristiano Ronaldo - Real Madrid
  Kocha Bora: Diego Simeone - Atletico Madrid
  Kipa Bora: Keylor Navas - Real Madrid (zamani Levante)
  Beki Bora: Sergio Ramos - Real Madrid
  Kiungo Bora wa ulinzi: Luka Modric - Real Madrid
  Kiungo Bora mshambuliaji: Andres Iniesta - Barcelona
  Mshambuliaji Bora: Cristiano Ronaldo - Real Madrid
  Mchezaji Bora wa Afrika: Yacine Brahimi - Granada
  Mchezaji Bora wa Amerika Kusini: Carlos Bacca - Sevilla
  Mchezaji Bora Chipukizi: Rafinha Alcantara - Barcelona (mkopo Celta 2013-14)
  Bao Bora: Cristiano Ronaldo (vs Valencia) - Real Madrid
  Mchezo wa Kiungwana: Ivan Rakitic - Barcelona (zamani Sevilla)
  Ronaldo's 'mule kick' against Valencia which won best goal
  Ronaldo ametwaa pia tuzo ya bao bora la msimu alilofunga dhidi ya Valencia hapa

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2810838/Cristiano-Ronaldo-clinches-La-Liga-best-player-award-ahead-Ballon-d-Or.html#ixzz3HUDGYv9z 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AMGARAGAZA 'VIBAYA' MESSI TUZO ZA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top