• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 22, 2014

  AZAM FC YAWEKA REKODI ‘BABU KUBWA’ LIGI KUU

  Na Nagma Khalid, DAR ES SALAAM 
  AZAM FC mwishoni mwa wiki imetimiza mechi 38 bila kufungwa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Shukrani kwake, beki Aggrey Morris aliyefunga bao hilo pekee kipindi cha kwanza kwa mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20 na Azam ikapanda kileleni mwa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu huu.
  Azam FC, sasa ina pointi 10 sawa na Mtibwa Sugar ya Morogoro, lakini timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na famili yake ina wastani mzuri zaidi wa mabao ya kufunga na kufungwa.
  Kikosi cha Azam FC kilichocheza mechi ya 38 bila kufungwa Jumamosi mjini Mbeya

  Februari 23, mwaka 2013 ndipo Azam FC ilifungwa kwa mara ya mwisho katika Ligi Kuu, ilipolala 1-0 mbele ya Yanga SC- unazungumzia misimu miwili iliyopita.
  Msimu uliopita Azam FC imekuwa bingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, bila ya kupoteza mchezo hata mmoja na sasa inaingia kwenye Raundi ya tano ya msimu huu wa ligi hiyo, bila kupoteza mechi.
  Azam FC imeshinda mechi tatu na kutoa sare mbili, kati ya mechi hizo, mbili imecheza ugenini, zote Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ambako ilivuna pointi nne, kwa sare ya 0-0 na Prisons na ushindi wa 1-0 na Mbeya City.
  Azam FC ilicheza mechi zake mbili za kwanza za Ligi Kuu nyumbani, Uwanja wa Azam Complex na kushinda 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting na 3-1 dhidi ya Polisi Morogoro.
  Rekodi ya kucheza mechi 38 bila kupoteza ni ya kujivunia na kama ingekuwa imewekwa na timu ‘za wananchi’- basi ingekuwa ikiimbwa kila siku kwenye vyombo habari.
  Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog anataka kuendeleza rekodi hiyo kwa kuhakikisha kwamba na msimu huu pia, Azam FC inamaliza Ligi bila kupoteza mechi.

  AZAM FC MECHI 38 BILA KUFUNGWA LIGI KUU

  Feb 23, 2013: Yanga SC 1-0 Azam FC
  Machi 9, 2013:  Azam 1-1 Polisi Moro
  Machi 27, 2013: Azam 3-0 Prisons
  Machi 30, 2013: Ruvu Shooting 0-1 Azam FC
  Aprili 11, 2013: Azam 1-1 African Lyon
  Aprili 14, 2013: Azam FC 2-2 Simba
  Aprili 26, 2013: Coastal Union 1-1 Azam FC
  Mei 11, 2013:  Azam FC 3-0 JKT Mgambo
  Mei 18, 2013: JKT Oljoro 0-1 Azam FC
  Agosti 24, 2013: Mtibwa Sugar 1 – 1 Azam FC
  Agosti 28, 13: Rhino Rangers 0-2 Azam FC
  Sept 14, 2013: Kagera Sugar 1-1 Azam FC
  Sepe 18, 2013: Azam FC 1-1 Ashanti United
  Sept 22, 2013: Azam 3-2 Yanga SC 
  Sept 29, 2013: Prisons 1-1 Azam FC
  Mei 5, 2013:   Coastal Union 0-0 Azam FC
  Okt 9, 2013: Azam FC 2-0 JKT Mgambo
  Okt 13, 2013: Azam FC 3-0 JKT Ruvu Stars
  Okt 19, 2013: JKT Oljoro FC 0 – 1 Azam FC
  Okt 28, 2013: Simba SC 1-2 Azam FC
  Nov 2, 2013: Azam 3-0 Ruvu Shooting
  Nov 7, 2013: Azam 3-3 Mbeya City
  Nov 25, 2014: Azam 1-0 Mtibwa Sugar
  Nov 29, 2014: Azam 1- 0 Rhino Rangers
  Feb 2, 2014: Azam 4-0 Kagera Sugar
  Feb 23, 2014: Azam 2-2 Prisons
  Feb 26, 2014: Ashanti United 0-4 Azam
  Machi 15, 2014: Azam FC 4-0 Coastal Union
  Machi 19, 2014: Yanga SC 1-1 Azam FC
  Machi 23, 2014: Azam FC 1-0 JKT Oljoro FC
  Machi 26, 2014: JKT Mgambo 0-2 Azam FC
  Machi 30, 2014: Azam FC 2-1 Simba SC
  Aprili 10, 2014: Ruvu Shooting 0-3 Azam FC
  Aprili 13, 2014: Mbeya City 1-2 Azam FC
  Aprili 19, 2014: Ruvu Stars 0-1 Azam FC
  Sept 20, 2014: Azam FC 3-1 Polisi Moro
  Sept 27, 2014: Azam FC 2-0 Ruvu Shooting
  Okt  4, 2014: Prisons 0-0 Azam FC
  Okt 18, 2014: Mbeya City 0-1 Azam FC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWEKA REKODI ‘BABU KUBWA’ LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top