• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 30, 2014

  ROBO FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND, MOURINHO APEWA WABISHI WA DARAJA LA KWANZA, LIVERPOOL NA BOURNEMOUTH

  KLABU ya Chelsea itakutana na Derby County katika Robo Fainali ya Kombe la Ligi, wakati Newcastle itapambana na Tottenham baada ya kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi, na mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City usiku wa jana. 
  Timu ya Alan Pardew imetinga Robo Fainali baada ya mabao ya Rolando Aarons na Moussa Sissoko kuwapa ushindi wa 2-0 dhidi ya City, ambayo jana imetimiza mechi tatu bila ushindi. 
  timu ya Eddie Howe, FC Bournemouth yenyewe imepewa vigogo wengine wa England, Liverpool na watasafiri hadi Pwani ya Kusini. 
  Jose Mourinho, kocha wa Chelsea atapambana na timu ya Daraja la kwanza, Derby County 

  ROBO FAIBALI KOMBE LA LIGI ENGLAND 

  Tottenham vs Newcastle 
  Derby vs Chelsea 
  Bournemouth vs Liverpool
  Sheffield vs Southampton
  Timu hizo mbili zinafahamiana vyema baada ya mwaka jana kukutana katika Kombe la FA, wakati Derby - ambayo iliitoa Fulham Uwanja wa Craven Cottage Jumanne itaikaribisha Chelsea huko Midlands. 
  Kocha wa Chelsea, Jose Marounho amepania kutwaa mataji yote England msimu huu na bila shaka kuanzia hatua hii ya Capital One Cup atahitaji kutumia wachezaji wake bora ili kupata matokeo mazuri.
  Mechi hizo zinatarajiwa kufanyika mwezi ujao, Desemba 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ROBO FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND, MOURINHO APEWA WABISHI WA DARAJA LA KWANZA, LIVERPOOL NA BOURNEMOUTH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top