• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 29, 2014

  KIPA UINGEREZA AJIGONGA VIBAYA KWENYE NGUZO YA LANGO AKIOKOA BAO KOMBE LA LIGI, AKIMBIZWA HOSPITALI PAPO HAPO

  KIPA wa Rangers, Steve Simonsen alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kujigonga kwenye nguzo ya lango huko Ibrox jana.
  Timu ya Ally McCoist ilikuwa mwenyeji wa timu ya Ligi Kuu, St Johnstone katika Robo Fainali ya Kombe la Ligi Scotland wakati Simonsen alipojiumiza mwenyewe katika harakati za kuokoa.
  Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 35 nafasi yake ilichukuliwa na Lee Robinson baada ya kutolewa uwanjani akiwa amebebwa kwenye machela mwanzoni mwa kipindi cha pili, kabla ya bao la kichwa la Lewis Macleod dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho kuamua mshindi.

  Kipa wa Rangers, Steve Simonsen akiwa amejigonga kichwa kwenye nguzo la lango wakati wa mechi dhidi ya St Johnstone

  Kocha wa Rangers, Ally McCoist alisema baada ya ushindi huo kwamba Simonsen anapatiwa matibabu hospitali baada ya kuumia akiokoa mchomo wa kichwa wa Brian Graham kipindi cha pili.
  The 35-year-old had to leave the pitch on a stretcher after the collision early in the second half at Ibrox
  Kipa huyo akiwa amebebwa kwenye machela kutolewa uwanjani kabla ya kukimbizwa hospitali
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPA UINGEREZA AJIGONGA VIBAYA KWENYE NGUZO YA LANGO AKIOKOA BAO KOMBE LA LIGI, AKIMBIZWA HOSPITALI PAPO HAPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top