• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 29, 2014

  BALOTELLI ATOKEA BENCHI NA KUIFUNGIA LIVERPOOL IKITINGA ROBO FAINALI KOMBE LA LIGI

  KLABU ya Liverpool imeichapa Swansea mabao 2-1 katika mchezo wa Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup usiku huu Uwanja wa Anfield.
  Jordan Henderson alipewa beji ya Unahodha, kocha Brendan Rodgers akifanya mabadiliko ya wachezaji tisa katika kikosi chake cha kwanza.
  Winga wa Swans, Marvin Emnes aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 65, kabla ya Mario Balotelli aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Rickie Lambert kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tano.
  Federico Fernandez alitolewa kwa kadi nyekundu dakika za mwisho kwa kumchezea rafu Philippe Coutinho kabla ya Dejan Lovren kuifungia Liverpool bao la ushindi dakika za majeruhi na kuwapeleka Wekundu hao Robo Fainali.
  Balotelli ametokea benchi usiku huu kuifungia Liverpool ikitinga Robo Fainali Kombe la Ligi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BALOTELLI ATOKEA BENCHI NA KUIFUNGIA LIVERPOOL IKITINGA ROBO FAINALI KOMBE LA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top