• HABARI MPYA

    Friday, October 10, 2014

    SIMBA SC: FATHER PAZI HAJAFUKUZWA NA WALA KOCHA WA OMAN HAJAPEWA KAZI, NI UZUSHI

    Na Princess Asia, JOHANNESBURG
    SIMBA SC imekanusha kumfukuza kocha wake wa makipa Iddi Pazi ‘Father’ na imesema haina mpango wa kumleta Choke Abeid kutoka Oman.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema; “Habari za kufukuzwa kocha wa makipa si kweli, na habari za kuletwa kocha wa Oman si kweli na imetusikitisha sana, sijui mmezitoa wapi hizi habari,”alisema Hans Poppe.
    Hata hivyo, Poppe hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo. Jana jioni ziliibuka habari kwamba, Simba SC imemtimua Fater Pazi na nafasi yake atachukua kocha wa makipa wa Oman, Choke Abeid. Ilielezwa Abeid ataungana na timu wakati wowote kuanza kazi kambini Afrika Kusini.
    Hans Poppe wa pili kulia amesema Simba SC haijafukuza kocha wa makipa

    Pazi aliachwa Dar es Salaam wakati Simba SC inaondoka juzi na baada ya kikosi kufika Afrika Kusini, kocha Mzungu wa nchini humo akaanza kazi ya kuwanoa makipa wa Wekundu hao wa Msimbazi.
    Simba SC ilianza mazoezi jana kwenye viwanja vya 
    Hoteli ya Eden Vale Petra mjini Johannesburg walipofikia na kesho watacheza mchezo wa kirafiki na wenyeji Orlando Pirates mjini Johannesburg.
    Simba ipo Afrika Kusini tangu juzi kwa ajili ya maandalizi yake ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 18, mwaka huu Dar e Salaam.
    Katika mchezo na Pirates, Simba SC itawakosa wachezaji wake walio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda, The Cranes- ambao wanatarajiwa kujiunga na wenao kuanzia Jumatatu.
    Hata hivyo, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na The Cranes yeye hatakwenda kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati ya wiki. 
    Wachezaji wa Simba SC walioko Stars ni; mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu.
    Simba SC itakuwa ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani.
    Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC: FATHER PAZI HAJAFUKUZWA NA WALA KOCHA WA OMAN HAJAPEWA KAZI, NI UZUSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top