• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 30, 2014

  YANGA SC WATUA ‘SALAMA SALMINI’ BUKOBA TAYARI KWA KAZI NA KAGERA SUGAR JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
  KIKOSI cha Yanga SC kimewasili salama mjini Bukoba mkoani Kagera, tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar Jumamosi.
  Yanga SC inayofundishwa na Mbrazil, Marcio Maximo itacheza na Kagera Sugar Jumamosi Uwanja wa Katiaba katika mfululizo wa Ligi Kuu, ikihitaji pointi tatu za kujiweka vizuri katika mbio za ubingwa.
  Yanga SC imewasili Bukoba mchana wa leo, ikitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambako jana ilicheza mchezo wa kirafiki na Ambassador ya Daraja la Pili mjini humo na kushinda 1-0, bao pekee la Said Bahanuzi.
  Yanga SC wakiwa kwenye basi lao baada ya kuwasili Bukoba

  Yanga SC yenye pointi 10 inafukuzana na Azam FC yenye pointi 10 pia na Mtibwa Sugar pointi 13 kileleni mwa Ligi Kuu msimu huu. Yanga SC ipo nafasi ya tatu kwa kuzidiwa wastani wa mabao na Azam FC.
  Yanga SC itashuka dimbani Jumamosi, ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa kwanza ugenini, baada ya kuichapa mabao 3-0 Stand United Uwanja wa Kambarage Shinyanga Jumamosi iliyopita.  
  Kagera inaingia kwenye mchezo huo, ikitoka kulazimishwa sare mbili mfululizo  nyumbani, kwanza na Stand United na Jumamosi iliyopita na Coastal Union ya Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WATUA ‘SALAMA SALMINI’ BUKOBA TAYARI KWA KAZI NA KAGERA SUGAR JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top