• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 30, 2014

  PETER SCHMEICHEL ASEMA MAN CITY 'WAMEKWISHAIPOTEZA' UNITED

  KIPA wa zamani wa Manchester United, Peter Schmeichel anaamini kwa sasa Manchester City ni klabu kubwa zadi ya wapinzani wao hao wa Jiji katokana na ubora wao siku za karibuni.
  Katika miaka yake minane ya kudaka Old Trafford, Schmeichel hakuwahi kupoteza mechi ya mahasimu wa Manchester hata moja na hakukuwa na shaka United ndio walikuwa 'babu kubwa' Jijini humo. 
  Lakini mtu mzima huyo mwenye umri wa miaka 50 sasa anafikiri uwiano wa nguvu umehamia City. "Katika miaka yangu kasha ya kwanza United, sikuwahi kuelewa upinzani na City. Liverpool na Leeds zilikuwa kubwa zaidi,’ amesema Schmeichel.
  "Sasa ni tofauti. Man City ni mabingwa, wametwaa taji lao la pili la Ligi Kuu msimu uliopita na labda kwa sasa ndiyo timu kubwa kuliko Manchester United katika maana ya matokeo, hivyo mambo yamebadilika,".
  Peter Schmeichel amesema Manchester City kwa sasa ni zaidi ya United

  Mshindi huyo wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya bado ni shabiki mkubwa wa United, ingawa anasema kucheza dhidi ya timu ya Sir Alex Ferguson akiwa Man City ilikuwa ni uzoefu mkubwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PETER SCHMEICHEL ASEMA MAN CITY 'WAMEKWISHAIPOTEZA' UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top