• HABARI MPYA

    Thursday, October 23, 2014

    PODOLSKI AING'ARISHA ARSENAL UGENINI LIGI YA MABINGWA

    ARSENAL imetoka nyuma na kushinda 2-1 katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini usiku huu. 
    Shukrani kwake, Lukas Podolski aliyetokea benchi ambaye alifunga bao la ushindi dakika ya 91 mjini Brussels, Ubelgiji baada ya The Gunners kutanguliwa kutunguliwa kwa bao la Andy Najar dakika ya 72.
    Lakini Kieran Gibbs aliisawazishia timu ya Arsene Wenger dakika ya 88 kabla ya Podolski kuleta ushindi. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Borussia Dortmund imeichapa 4-0 Galatasaray nchini Uturuki.
    Kikosi cha Anderlecht kilikuwa: Proto, Vanden Borre, Mbemba, Deschacht, Acheampong, Tielemans, Defour, Najar, Praet/Dendoncker dk88, Conte na Cyriac/Suarez dk83. 
    Arsenal: Martinez, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Flamini/Oxlade-Chamberlain dk74, Sanchez, Ramsey, Wilshere/Podolski dk84, Cazorla na Welbeck/Campbell dk74. 

    Lukas Podolski akishangilia na mchezaji menzake Per Mertesacker baada ya kuifungia bao la ushindi Arsenal

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2803928/Anderlecht-1-2-Arsenal-Lukas-Podolski-fires-home-injury-time-Gunners-score-two-goals-two-minutes-steal-dramatic-victory.html#ixzz3GuYZWh2B 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PODOLSKI AING'ARISHA ARSENAL UGENINI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top