• HABARI MPYA

  Friday, October 31, 2014

  PIGO MAN CITY KUELEKEA MECHI NA MAN UNITED, SILVA AUMIA GOTI NA ATAKUWA NJE WIKI TATU

  KIUNGO David Silva hatacheza keshokutwa mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester katokana na maumivu ya goti.
  Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema kiungo huyo wa Hispania atakuwa nje kwa wiki tatu au nne baada ya kuumia goti lake Jumatano usiku katika mchezo wa Kombe la Ligi, England maarufu kama Capital One Cup. 
  Man City ilifungwa 2-0 na kutolewa na Newcastle United, iliyotinga Robo Fainali.
  Silva hataukosa mchezo huo wa Jumapili wa Ligi Kuu ya England dhidi ya mahasimu Man United pekee, bali atakosa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki ijayo na CSKA Moscow Uwanja wa Etihad. 
  David Silva atakosekana katika mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester dhidi ya United kutokana na maumivu ya goti
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO MAN CITY KUELEKEA MECHI NA MAN UNITED, SILVA AUMIA GOTI NA ATAKUWA NJE WIKI TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top