• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 25, 2014

  REAL MADRID YAICHAPA BARCELONA 3-1 LA LIGA, MESSI ATIWA MFUKONI...PEPE AFUNGA

  REAL Madrid imeifumua mabao 3-1 Barcelona katika mchezo wa La Liga jioni ya leo Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid.
  Mbrazil Neymar alitangulia kuifungia Barcelona dakika ya nne, kabla ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Mreno Cristiano Ronaldo kusawazisha kwa penalti dakika ya 35, kufuatia Gerard Pique kuunawa mpira kwenye boksi.
  Beki Mreno, Pepe akaifungia Real Madrid bao la pili dakika ya 51, kabla ya mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya 61.
  Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo, Kroos, Modric/Arbeloa dk89, Isco/Illarramendi dk83, James, Ronaldo na Benzema/Khedira dk86. 
  Barcelona: Bravo, Alves, Pique, Mascherano, Mathieu, Xavi/Rakitic dk60, Busquets, Iniesta/Roberto dk71, Messi, Suarez/Pedro dk69 na Neymar.

  Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga katika El Clasico baina ya Real Madrid na Barcelona leo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2807812/Real-Madrid-3-1-Barcelona-Luis-Suarez-debut-ends-defeat-Lionel-Messi-beaten-Cristiano-Ronaldo-El-Clasico.html#ixzz3HBLlFdfB 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAICHAPA BARCELONA 3-1 LA LIGA, MESSI ATIWA MFUKONI...PEPE AFUNGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top