• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 25, 2014

  AZAM FC YACHAPWA CHAMAZI, JKT YAVUNJA REKODI YAO YA KUTOFUNGWA MISIMU MIWILI

  BAO pekee la mshambuliaji Samuel Kamuntu limeipa JKT Ruvu ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.  
  Kamuntu alifunga bao hilo dakika ya 44, akimalizia krosi ya Najim Magulu aliyepasiwa na Jabir Aziz. Mshambuliaji huyo aliingia uwanjani dakika ya 10, kuchukua nafasi ya Iddi Mbaga aliyeumia mapema tu.
  Huo ni ushindi wa pili mfululizo wa JKT katika Ligi Kuu, baada ya Jumamosi iliyopita kuichapa Prisons 2-1 na sasa inafikisha pointi saba baada ya kufungwa mechi mbili, sare moja na kushinda mbili.
  Kamuntu wa pili kushoto akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao pekee 

  Azam FC inafungwa kwa mara ya kwanza baada ya mechi 38 mfululizo ndani ya misimu miwili bila kupoteza mechi na inabaki na pointi zake 10, sawa na Mtibwa na Yanga SC.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gadiel Michael, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Gudence Mwaikimba dk68, Erasto Nyoni, Didier Kavumbangu, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Farid Mussa/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk51. 
  JKT Ruvu; Jackson Chove, Ramadhani Shamte, Napho Zuberi, Madenge Ramadhani, Mohammed Faki, George Minja, Amos Mgisa/Nashon Naftali dk46, Jabir Azizi, Iddi Mbaga/Samuel Kamuntu dk10, Najim Magulu na Ally Bilal/Emmanuel Pius.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA CHAMAZI, JKT YAVUNJA REKODI YAO YA KUTOFUNGWA MISIMU MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top