• HABARI MPYA

    Thursday, October 09, 2014

    BALOTELLI LIVERPOOL NI NAFASI YA MWISHO, ASEMA MANCINI

    KOCHA Roberto Mancini anaamini Mario Balotelli kutua Liverpool ni nafasi yake ya mwisho kuthibitisha uwezo wake katika klabu kubwa- na mshambuliaji huyo wa Wekundu hao anafahamu hilo. 
    Mshambuliaji huyo wa Italia bado anahaha kuonyesha umuhimu wake Anfield tangu atue kwa dau la Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan msimu huu na ameweza kufunga bao moja akiwa na timu hiyo hadi sasa.
    Mancini, ambaye alifanya kazi na mchezaji huyo katika klabu za Inter Milan na Manchester City, anatumai Balotelli  anaweza kuanza kufanya vizuri Ligi Kuu England.
    Mario Ballotelli kuwa kwake Liverpool ni nafasi yake ya mwisho kudhihiriha uwezo wake katika klabu kubwa kwa mujibu wa Roberto Mancini

    Mancini amesema: "Mario ni kijana mzuri, lakini anafahamu kwamba Liverpool inaweza kuwa nafasi yake ya mwisho kuthibitisha anachoweza kufanya uwanjani. Ni nafasi yake ya mwisho. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALOTELLI LIVERPOOL NI NAFASI YA MWISHO, ASEMA MANCINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top