• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 23, 2014

  YANGA SC WATOA SARE NA CDA YA DARAJA PILI DOM LEO, KASEJA NA BARTHEZ WADAKA KWA ZAMU, TEGETE NA BAHANUZI WAKOSA MABAO YA WAZI

  Na Paul Mabeja, DODOMA
  YANGA SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na CDA ya Dodoma katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma jioni ya leo.
  Kocha Mbrazil, Marcio Maximo leo aliwaanzisha wachezaji wake wa akiba, ambao walishindwa kufurukuta mbele ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.
  Shambulizi la maana ambalo Yanga SC walifanya kipindi cha kwanza ilikuwa dakika ya 40, baada ya Mganda Hamisi Kiiza kupata krosi nzuri na kumpa pasi nzuri pia Jerry Tegete ambaye katika mastaajabu ya wengi, akapiga nje.
  Na kipindi cha pili, Said Bahanuzi naye alipoteza nafasi ya kufunga dakika ya 85 baada ya kuunganishia nje kwa shuti kubwa krosi ya Salum Telela.
  Jerry Tegete amekosa bao la wazi leo Yanga SC ikitoka 0-0 na CDA mjini Dodoma
  CDA inayofundishwa na Juma Ikaba, mchezaji wake wa zamani, pamoja na Reli Morogoro na Ushirika ya Moshi, inajiandaa na Ligi Daraja la Pili, inayotarajiwa kuanza mwezi ujao, wakati Yanga ilikuwa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United mjini Shinyanga mwishoni mwa wiki.
  Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Juma Kaseja/Ally Mustafa ‘Barthez’, Salum Telela, Amos Abel, Patrick Ngonyani, Rajab Zahir, Said Juma ‘Kizota’, Omega Seme, Nizar Khalfan, Hussein Javu, Jerry Tegete na Hamisi Kiiza/Said Bahanuzi.
  CDA; Francis Ishengoma, Aaron Michael/Hamisi Athumani, Peter Ngoyi, Suleiman Msuya, Shaaban Zanka, Ibrahim Ndecha, Hamisi Moru, Hamisi Hilal, Titus Stanley, Mohamed Neto/Hussein Kunga na Idrisa Rajab/Ally Lutavi.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WATOA SARE NA CDA YA DARAJA PILI DOM LEO, KASEJA NA BARTHEZ WADAKA KWA ZAMU, TEGETE NA BAHANUZI WAKOSA MABAO YA WAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top