• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 27, 2014

  NAHODHA BAFANA, ORLANDO PIRATES AUAWA KWA RISASI

  Na Mwandishi Wetu, JOHANNESBURG
  KIPA wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ na klabu ya Orlando Pirates, Senzo Meyiwa (pichani) amepigwa risasi na kufariki dunia, Polisi nchini hapa imethibitisha jana.
  Polisi imethibitisha mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 27 alithibitika kufa alipofikishwa katika hospitali East Rand, huko Gauteng.
  Taarifa rasmi za shambulizi lake bado hazijapatikana na ofa nzuri imetangazwa kwa yeyote atakayetoa maelezo.
  Nahodha huyo wa klabu na timu ya taifa, Meyiwa aliichezea Orlando Pirates juzi Uwanja wa Orlando wakishinda 4-1 kwenye Robo Fainali ya michuano ya mtoano ya Telkom dhidi ya Ajax Cape Town. Pumzika kwa amani Meyiwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAHODHA BAFANA, ORLANDO PIRATES AUAWA KWA RISASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top