• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 22, 2014

  SIMBA SC WAIFUATA PRISONS MBEYA KWA ARI KUBWA

  Na Samira Said, DAR ES SALAAM
  IKIWA chini ya Mzambia, Patrick Phiri, Simba SC ya Dar es Salaam iliondoka leo asubuhi kuelekea mkoani Mbeya kwa lengo la kwenda kuivaa Prisons katika mechi ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana jioni, Phiri, alisema kuwa kikosi chake kinakwenda moja kwa moja Mbeya na hakitacheza mechi nyingine ya kirafiki.
  Phiri alisema kuwa kikosi chake kiko katika morali ya kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu na kurejesha amani kwenye klabu yao.
  Simba SC iko safarini kwenda Mbeya

  “Tutaondoka wote, tunaenda Mbeya kwa kazi moja ya kusaka matokeo mazuri,” alisema kwa kifupi kocha huyo.
  Aliwataja wachezaji waliobaki jijini ni majeruhi ambao hawakucheza na hawajakuwepo katika orodha ya mchezo wa watani wa jadi, Yanga ambao ulifanyika Jumamosi iliyopita.
  Simba itashuka dimbani ikiwa na pointi nne ambazo wamepata kutokana na sare nne dhidi ya Coastal Union, Polisi Morogoro, Stand United na Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAIFUATA PRISONS MBEYA KWA ARI KUBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top