• HABARI MPYA

    Wednesday, October 22, 2014

    TARSIS MASELA KUZINDUA ALBAMU KALI INAITWA ACHA HIZO NOVEMBA 21 DAR

    Na Samira Said, DAR ES SALAAM
    MWIMBAJI wa muziki wa Dansi, Tarsis Masela, anatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yake ya kwanza iitwayo Acha Hizo utakaofanyika Novemba 21 kwenye Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) ulioko jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza jana jijini, Masela, ambaye pia ni mwanamuziki na Rais wa bendi ya Akudo, alisema kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo saba na zina ujumbe mbalimbali ambao unalenga kuelimisha jamii.
    Masela alizitaja nyimbo zilizoko katika albamu hiyo kuwa ni pamoja na Tabia Mbaya ambayo amemshirikisha ‘Mfalme’ wa taarabu, Mzee Yusuph, Chaguo Langu, Nimevumilia (Lady Jay Dee).
    Tarsis Masela kushoto akizungumza na Waandishi wa habari leo. Kulia ni Meneja wake, Ray Matata

    Alisema nyimbo nyingine ni Vidole Vitatu, Penzi Langu Limezidi Asali, Mwiko na Tusiachane.
    “Hii ni albamu yangu ya kwanza tangu nianze muziki, nimeshirikisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya na taarabu ili kuifanya iwe na ladha tofauti na ubora wa juu,” alisema Masela.
    Aliongeza kuwa katika uzinduzi wake atasindikizwa na wasanii mbalimbali ambao kwa sasa wako kwenye mazungumzo ya mwisho ili kulifanya onyesho hilo liwe na ubora wa aina yake.
    Naye Meneja wa msanii huyo, Ray Matata,alisema kuwa maandalizi ya onyesho hilo yanaendelea vizuri na wamejipanga kufanya mapinduzi kwenye muziki wa dansi.
    Matata alisema kwamba Masela ameonyesha nia na amewataka wadau wa sanaa ya muziki kujiandaa kushuhudia onyesho lenye ubora wa kimataifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TARSIS MASELA KUZINDUA ALBAMU KALI INAITWA ACHA HIZO NOVEMBA 21 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top