• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 25, 2014

  ‘FUNDI MKUDE’ ATAKUWEPO OFISINI SIMBA NA MTIBWA JAMHURI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Jonas Mkude hayuko kwenye nafasi ya kucheza mechi ya leo baina ya Simba SC na wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, lakini atakuwa fiti kwa asilimia 100 katika mechi ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
  Jonas Mkude (pichani) jana alianza mazoezi mepesi baada ya kuwa mapumziko tangu alipoumia kwenye mechi na Yanga SC Jumamosi iliyopita na mwenyewe anasema anajisikia nafuu.
  ‘Fundi Mkude’ alitolewa dakika ya 60 kumpisha Pierre Kwizera baada ya kuumia bega katika mechi dhidi ya Yanga SC, iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana.
  Awali, Mkude alikuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na maumivu ya goti, lakini baada ya kupona akakutana na ‘zahma’ nyingine ya bega- ila kwa sasa yuko fiti na tarajia Jumamosi atacheza Uwanja wa Jamhuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ‘FUNDI MKUDE’ ATAKUWEPO OFISINI SIMBA NA MTIBWA JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top