• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 27, 2014

  SIMBA SC YAENDA KUWEKEA KAMBI MAKAMBAKO, KIEMBA, CHANONGO WAREJESHWA DAR KWA KUCHEZA CHINI YA KIWANGO, KISIGA NIDHAMU

  Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inaondoka Mbeya asubuhi ya leo kwenda kuweka kambi Makambako, Iringa kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa wiki.
  Simba SC itamenyana na vinara wa Ligi Kuu, Mtibwa Sugar Jumamosi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mfululizo wa ligi hiyo.
  Hata hivyo, kambi hiyo itawakosa wachezaji watatu, Shaaban Kisiga ‘Malone’, Amri Kiemba na Haroun Chanongo ambao watarejea Dar es Salaam leo kwa sababu mbalimbali.
  Shaaban Kisiga (kulia) amerejeshwa Dar es Salaam na wenzake wawili, Amri Kiemba na Haroun Chanongo 

  Kisiga anarejeshwa Dar es Salaam kwa tuhuma za kutoa majibu ya kifedhuli kwa uongozi kabla ya mchezo na Prisons Jumamosi, wakati Kiemba na Chanongo ni kucheza kwa kiwango cha chini.
  BIN ZUBEIRY inafahamu wachezaji hao wametakiwa kuripoti ofisini kwa Rais, Evans Elieza Aveva Ijumaa mjini Dar es Salaam kwa majadiliano ya kina.
  Kocha wa Simba SC, Patrick Phiri amesema kwamba timu ikiwa Iringa, itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Lipuli.
  Jana jioni, wachezaji, viongozi wa juu na benchi la ufundi la Simba walikuwepo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kuwasoma Mtibwa walioiadhibu Mbeya City mabao 2-0.
  Simba SC ilitoa sare ya kufungana bao 1-1 na Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu uliotangulia Jumamosi mjini hapo. Hiyo ilikuwa sare ya tano mfululizo katika mechi tano za Ligi Kuu msimu huu kwa Wekundu hao wa Msimbazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDA KUWEKEA KAMBI MAKAMBAKO, KIEMBA, CHANONGO WAREJESHWA DAR KWA KUCHEZA CHINI YA KIWANGO, KISIGA NIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top