• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 24, 2014

  YANGA SC YAANZA KUIPOTEZA SMBA SC MTANI JEMBE 2

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAKATI shindano la ‘Nani Mtani Jembe2’ likiendelea, baina ya wakongwe wa Soka hapa nchini Yanga na Simba, Yanga wameendelea kufanya vema katika kampeni ya kuvutana ambayo mil 80 zinawaniwa na mmoja wa vigogo hao ambaye atang’ara kumzidi mwenzake.
  Kampeini hiyo, inayoratibiwa na wadhamini wakuu wa timu hizo bia ya Kilimanjaro Premium Lager ilianza rasmi mwanzoni mwa mwezi huu huku ikishirikisha michezo mbalimbali kama kuvuta kamba, kupiga danadana na mingineyo kwa viongozi na mashabiki wa timu hizo.

  Timu hizo, zinashindania kitita hicho cha sh mil 80, ambazo zimetengwa mil 40 kwa kila timu, huku mashabiki wa timu hizo wakitumia fursa hiyo kuzipatia timu zao pesa kutoka kwa timu pinzani kwa kunywa bia hiyo, ambapo chini ya kizibo kutakuwa na namba ambayo shabiki ataandika jina la timu kwenda namba 15415.
  Kwa mujibu wa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, mpaka sasa Yanga mpaka kufikia juzi Yanga alikuwa anaongoza katika kuvutana ambapo anajumla ya Mil 40,330,000 huku Simba ambao ambao ni mabingwa watetezi wakivuna sh 39,670,000.
  Kavishe alisema, kampeni hiyo ya aina yake, ambayo inawakutanisha wakongwe hao wa Soka hapa nchini, mbali na ushindani pia inawapa fursa wapenzi na mashabiki wa timu hizo kuwa kitu kimoja katika kuendeleza umoja wao licha ya kuwa na ushindani dimbani.
  Alisema, msimu huu wamelibolesha shindano hilo, kutokana na kuwepo kwa vitu mbalimbali, kama dakika 30 za kipindi cha Kili Chat ambacho hurushwa kila Alhamis saa 3:00 usiku katika kituo cha runinga cha EATV ikiwa na lengo la kuzungumzia kampeini hiyo kupitia watu mbalimbali kama wasanii na wengineo. “Kilimanjaro Premium Lager kama mnavyofahamu ni bia ya kiburudisho tosha, na ndio maana imejikita katika masuala mbalimbali ya kimichezo na hata burudani pia, kwani mbali na mtani jembe pia tuko katika muziki, riadha na mambo mengine,”alisema na kuongeza kwa kuwataka wapenzi wa soka hasa Simba na Yanga kutazama kipindi hicho ili kujua mwenendo wa timu zao.
  Aliongeza kuwa, kampeini hiyo inayotarajiwa kufikia tamati Disemba 13 kwa kuzikutanisha timu hizo dimbani inaendelea kufanywa katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwenye Mikoa ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam pamoja na Mikoa mingine mingi.
  Katika kampeni hiyo inetengwa shilingi milioni 100 ambapo shilingi milioni 80 zinashindaniwa na timu hizo kupitia kura za mashabiki huku sh milioni 20 ikiwa ni zawadi ya mechi ya Nani MtaninJembe ambapo mshindi atapata shilingi milioni 15 na atakayefungwa atapata kifuta jasho sh milioni 5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAANZA KUIPOTEZA SMBA SC MTANI JEMBE 2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top